Kuandaa: dakika 60
Mapishi: dakika 10
Mapishi: dakika 10
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mahitaji
- Mchele kg 1
- Tui la nazi vikombe2
- Yai 1
- Sukari ½ kikombe
- Iliki kijiko 1 cha chakula iliyosagwa
- Unga wa ngano vijiko 2 vya chakula
- Mafuta ya kula
- Hamira ½ kijiko cha chai
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Unaweza kuongeza viungo unavyopenda kwenye vitumbua ili kuvipa ladha tamu zaidi. Hakikisha tu unakuwa makini wakati wa kukaanga, maana huwa vinaharibika na kutoka vibichi kwa ndani usipoviacha muda wa kutosha kwenye mafuta.- Loweka mchele kwa muda usiopungua masaa 4, kisha chuja maji. Weka mchele na tui la nazi kwenye blender. Saga pamoja ili mchanyiko ulainike usiwe na chenga.
- Weka Iliki, hamira na unga wa ngano kwenye mchanganyiko ulio kwenye blender. Saga pamoja hadi mchanyiko uwe uji uliochanganyika vizuri. Mimina mchanganyiko kwenye bakuli. Funika vizuri kisha acha uumuke kiasi, ukiumuka weka sukari na yai kisha changanya vizuri.
- Weka chuma cha kuchomea vitumbua jikoni, moto usiwe mkali sana. Weka mafuta kidogo kwenye mashimo ya chuma cha kuchomea – kijiko baada ya kingine. Mafuta yakipata moto, pakua uji kwa kutumia upawa kisha jaza mashimo ya kukaangia virutumbua. Hakikisha kitumbua kinaiva vizuri na kukauka kabla ya kugeuza upande mwingine. Weka mafuta upande wa pili wa kitumbua, acha kikauke vizuri na kuwa na rangi ya kahawia. Toa kitumbua na weka pembeni. Rudia hatua hii hadi uji wa vitumbua uishe.
- Tenga vitumbua na ujirambe. Unaweza kula vikiwa vya moto au vya baridi
No comments:
Post a Comment