Mahitaji
- Nyama kilo 1
- Mafuta ya olive vijiko 3 vya chakula kwa ajili ya kulowekea
- Kitunguu saumu
- Tangawizi iliyosagwa vijiko 3
- Pilipili manga
- Papai bichi
- Siki nyeupe vijiko 2
- Chumvi
- Binzari kijiko 1
- Majani ya giligiliani kijiko 1
- Mdalasini kijiko 1
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
- Kata nyama vipande vikubwa kisha osha mara moja tu.
- Weka viungo kwenye nyama - kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga, papai bichi, mdalasini, binzari, siki, giligiliani, chumvi. Changanya vizuri viungo viingie vizuri kwenye nyama.
- Viungo vikishachanganyika vizuri mimina mafuta kwenye nyama. Mafuta haya ni kwa ajili ya kulowekea nyama.
- Weka nyama kwenye fridge kwa muda wa masaa mawili ili viungo vishike vizuri.
- Baada ya masaa mawili, anza kutunga nyama kwenye miti ya kuchomea tayari kwa kuchoma
- Ni vizuri kuchoma mshikaki kwa kutumia jiko la mkaa lakini unaweza
kutumia jiko lolote lile - oven au nishati yoyote unayopendelea. Cha
msingi hakikisha moto uwe wa wastani ili nyama iive vizuri.
Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa, nyama inatakiwa kuiva vizuri nje na ndani. Moto mkali utababua nyama kwa nje na kuzuia kuiva vizuri ndani. Kama unatumia jiko la mkaa ni vizuri kugeuza mara kwa mara ili nyama ipate kuiva vizuri pande zote. Kama unatumia Oven huna haja ya kugeuza maana ni rahisi joto kuingia kwa uwiano mzuri kwenye nyama.
- Choma nyama kwa kugeuza geuza mpaka mishikaki iive vizuri.
- Jirambe.
No comments:
Post a Comment