Mahitaji
- Kilo 1 ya vipapatio vya kuku (chicken wings)
- Vitunguu saumu 4, menya kisha saga
- Vijiko 3 vikubwa vya asali
- Kijiko 1 kikubwa cha soy sauce, hii utapata supermarket au maduka ya viungo vya chakula
- Kijiko 1 kidogo cha pilipili (kama hupendi pilipili unaweza kuacha kutumia hii)
- Kijiko 1 kidogo cha pilipili manga, ya unga au saga vizuri
- Mafuta ya kula
- Limao au ndimu 1
- Chumvi
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
- Andaa vipapatio vya kuku – kata ncha (mie huwa situmii ncha), osha vizuri kisha weka kwenye chombo kilicho safi. Kamulia limao, weka chumvi ½ kijiko cha chai na pilipili manga. Koroga vizuri kwa mikono hadi zichanganyike vizuri. Hifadhi kwenye jokofu au sehemu yenye ubaridi kiasi kwa masaa 2 ili viungo vichanganyike na nyama vizuri. Kama huna muda unaweza kupika moja kwa moja.
- Weka kikaangio chenye mafuta jikoni. Mafuta yakipata moto weka kuku – geuza inapobidi. Acha waive vizuri kisha toa hifadhi pembeni.
- Kwenye kikaango tofauti (au kama unatumia chombo ulichokaangia kuku ni sawa pia) weka mafuta ya kula, bandika kwenye moto mdogo. Mafuta yakipata moto weka kitunguu saumu. Koroga na acha kiive hadi kianze kubadilika rangi, hakikisha hakiungui. Weka asali, soy sauce, na pilipili. Koroga vizuri. Acha vichemke na kuchanganyika kwa dakika 1.
- Weka vipapatio vya kuku (chicken wings), koroga vizuri zaidi. Ongeza moto ili asali na soy sauce vitoe povu kiasi, na kutoa hali ya kama kuungua na kunata.
- Toa chicken wings na anza kula.
No comments:
Post a Comment