Monday, 27 April 2015

FIRIGISI NA NDIZI ZA KUKAANGA

JUMAPILI-15
 Jumapili nilipata mgeni ikabidi niingie jikoni kumuandalia chakula cha mchana.Chakula kilikuwa firigisi na ndizi za kukaanga na salad kidogo.Nilihitaji vitunguu na karoti kama zinavyoonekana pichani.
 Firigisi zenyewe
Nikaweka sufuria jikoni na mafuta ya kupikia,mie natumia mafuta ya alizeti.
Mafuta yalipopata moto nikatia vitunguuu nikavikaanga mpaka vikawa brown.
Nikaweka firigisi zangu,unaweza kuzikata vipabde vidogo vidogo ila mie nilipendelea kuweka kama vilivyo.Nikaziacha zichemke kidogo kama dk 5 hivi…
Kisha nikatia limao,sikuongeza maji hata kidogo maana sikuwa nahitaji mchuzi.
Baada ya hapo nikaweka chicken masala ya aina hii naipenda sana maana ina harufu na ladha tamu sana.Huu ni mchanganyiko wa karafuu,tangawizi,kitunguu saumu,pilipili,chumvi,mdalasini,binzari,pilipili manga n.k
Nikaweka kijiko kimoja
Nikakoroga na kuongeza maji kidogo,chumvi kisha nikafunikia ziweze kuchemka na kuiva vizuri.
Baada ya dk 10 hivi nikaweka karoti na kukoroga kwa dk 1 kisha nikaipua zikiwa tayari zimeiva.
Pia nikakaanga ndizi kwa kuanza kuweka frying pan jikoni na mafuta ya kupikia.
 Ndizi niliziweka chumvi kabisa.
Mafuta yalipopata moto nikaweka ndizi na kuzikaanga.Zilipokuwa tayari nikaipua tayari kumuandalia mgeni chakula.
Ni chakula kitamu,haraka na rahisi kuandaaa…tayari kwa kuliwa.

No comments:

Post a Comment