Mahitaji
- Mayai yaliyochemshwa 6
- Nyama ya kusaga kilo moja
- Tangawizi na kitunguu saumu vilivyosagwa kijiko kimoja kikubwa
- Pilipili mbichi ya kusagwa 1
- Mafuta ya kupikia vijiko 2 vikubwa
- Unga wa mahindi kijiko kimoja kikubwa
- Dania ya unga robo kijiko cha chai
- chumvi kiasi
- Bizari ya manjano robo kijiko cha chai
1.Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.
2.Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri .
3.Ukisha
maliza yote panga kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni
nyunyizia mafuta kidogo na choma moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.
4.Yakishaiva epua na kisha ukate kama ilivyo kwenye picha .Tayari kuliwa .
No comments:
Post a Comment