Chicken fried rice
- Minofu ya kuku
- Wali uliopikwa na kukaa siku nzima (Kiporo)
- Mafuta ya kula
- Kitunguu maji
- Karoti
- Pilipili hoho
- Bizari
- Pilipili manga
- Green beans
- Chumvi
- Njegere
- Maji
- Mayai
- Soy sause
- Vitunguu vya kijani
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
- Pika wali kisha weka kwenye jokofu. Au kama una wali uliobaki siku iliyopita (kiporo) unaweza kutumia pia. Cha msingi wali uwe umeshaiva na kukaa kwa muda kabla ya kuanza mapishi haya.
- Tengeneza kuku. Kama nyama ya kuku ina mifupa, tenganisha minofu kisha kata vipande vidogo vidogo.
- Changanya vipande vya kuku na pilipili manga, bizari na chumvi. Changanya hadi uwiano uwe sawia.
- Weka chungu jikoni kisha kaanga kuku hadi awe kahawia. Akiiva, weka pembeni na funika vizuri asipoe.
- Bandika sufuria au kikaango. Weka kitunguu maji, kitunguu saumu, njegere, pilipili hoho, green beans na carrot. Koroga kwa muda wa dakika 2.
- Pasua mayai, mwagia kwenye mboga kisha koroga haraka haraka ili vichanganyike vizuri.
- Ongeza mafuta kidogo kwenye mboga.
- Weka wali kwenye mboga. Koroga ili uchanganyikane na mboga. Weka kuku, endelea Kukoroga takribani dakika 2 hadi 3.
- Ongeza soy sause kwenye chakula, koroga vizuri ichanganyikane na chakula mpaka maji maji yakauke kwenye chakula na wali uwe na rangi ya kahawia.
- Katia vitunguu vya majani kwa juu na upakue.
- Hapo chakula chako kitakua tayari na anza kujiramba.
No comments:
Post a Comment