Kuandaa: dakika 10
Mapishi: dakika 18
Mapishi: dakika 18
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Mahitaji
- Dagaa ½ kilo
- Vitunguu vikubwa 2
- Nyanya 4
- Pilipili hoho 1
- Karoti 1
- Nazi 1
- Vitunguu swaumu 1
- Chumvi ½ kijiko cha chai
- Mafuta ya kula
- Ndimu 1
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
- Anza kuandaa dagaa – kata vichwa, toa matumbo, osha na kisha weka vizuri kwenye sufuria.
- Andaa kitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti. Osha, kata vipande vidogo tayari kwa mapishi.
- Andaa tui la nazi – vunja nazi, kuna na kisha kamua tui zito na hifadhi vizuri pembeni.
- Weka sufuria ya kupikia jikoni, kisha mimina mafuta ya kula kiasi. Subiria yapate moto vizuri.
- Weka vitunguu kwenye sufuria. Koroga ili kufanya viive vizuri.
- Kabla vitunguu havijaiva vizuri, weka dagaa. Koroga na kukaanga vizuri dagaa.
- Dagaa wakianza kukauka kamulia ndimu juu yake. Koroga kiasi kisha weka pilipili hoho na karoti. Endelea kukoroga.
- Weka nyanya kwenye dagaa. Endelea kukoroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziive vizuri na mvuke na kuwa laini.
- Nyanya zikiiva unaweza kuziponda ili kupata rojo nzuri.
- Weka chumvi unayoona inafaa kutokana na kiwango cha mboga.
- Ongeza tui zito la nazi, endelea kukoroga ili tui lisikatike. Acha tui lichemke hadi liishe na ubaki mchuzi mzito.
- Unaweza kuepua dagaa wako na kujiramba.
No comments:
Post a Comment