Saturday, 18 April 2015

KUKU WA KUOKA ALIYEPAKWA JUISI YA CHUNGWA


Mahitaji

Viungo vya kuku
  • Paja za kuku 4
  • Mfuko mkubwa mgumu wa nailoni wa kuhifadhia chakula
  • Ujazo war obo tatu (3/4) wa kikombe cha juisi fresh ya chungwa –  machungwa 2
  • Vijiko 2 vya orange zest
  • Kijiko 1 cha chai cha chumvi
  • Vijiko 2 vya chai vya pilipili manga
  • Kijiko 1 cha chai cha majani ya mnanaa yaliyokatwa (Mint leaves)
  • Kijiko 1 ½  cha majani ya basil
  • Vijiko 3 vya balsamic vinegar nyeupe
  • Kitunguu maji 1 kilichokatwa vipande
  • Kijiko 1 cha mbegu za celery
 Viungo vya supu ya chungwa
  • Kijiko 1 cha mafuta ya zeituni (olive oil)
  • Kitunguu maji 1 kilichokatwa vipande
  • Kijiko 1 kidogo cha tangawizi iliyokata
  • ½ kikombe cha marmalade ya chungwa
  • ¼ kikombe ya pilipili (sweet chili sauce)
  • Kijiko 1 cha balsamic vinegar nyeupe
  • ¼ kikombe cha marinade iliyochunjwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuandaa kuku
  • Changanya viungo vyote kwenye mfuko mgumu wa nailoni – weka kuku pia – kisha hifadhi kwenye jokofu kwa muda wa masaa 6 hadi 8. 
  • Baada ya masaa 8, andaa oven yako kwenye joto la 350°F au (kama 180°C).
  • Toa kuku kwenye mfuko, muweke kwenye chombo cha kuokea kwenye oven, na kisha weka kwenye oven kwa muda wa dakika 45.
  • Muda ukifika, toa kuku kwenye oven, nyunyuzia sauce ya chungwa (maelezo yapo hapa chini), kisha rudisha kwenye oven kwa muda wa dakika 15 hadi 20. Uwe unaichungulia mara kwa mara na kuigeuza ili ipate kuenea vizuri.
  • Baada ya muda, weka tayari kwa ajili ya kuliwa.
Kuandaa Supu ya chungwa
  • Weka kikaangio jikoni, ongeza mafuta ya kula (Olive oil) halafu acha yapate moto.
  • Mafuta yakishapata moto, weka kitunguu na kisha koroga. Ongeza tangawizi. Kaanga kwa muda wa dakika 3.
  • Ongeza viungo vilivyosalia, punguza moto uwe wa wastani kisha acha viive, takribani dakika 15. Ukimaliza ongeza sauce kwenye kuku baada ya dakika 45 za mapishi ya kuku kuisha (Maelezo hapo juu)
Kuku wa Chungwa
Kuku wa chungwa kwenye Oven

No comments:

Post a Comment