Mahitaji
- Mapaja 4 ya kuku (Tumia idadi unayohitaji kukidhi mahitaji yako)
- Maggi cube
- Chumvi
- Kitunguu saumu 1 (Menya, kisha saga kiwe laini au tumia cha unga)
- Mafuta ya kula (Nimetumia olive oil, ila unaweza kutumia pia mafuta mengine yanayotokana na mimea au samaki)
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Ukihitaji kufurahi na una muda mzuri wa kuandaa kuku, basi haya mapishi yatakuwa mazuri kwako. Ni chakula kizuri kuandaa sababu unachokipata kinaendana na muda wako uliotumia kuandaa chakula. Kwenye chakula tumetumia ndizi mzuzu na viazi vilivyo kwenye mboga za majani. Unaweza kupata maelezo yake hapa. Ukimaliza, utakuta chakula hiki kinakusubiria:- Andaa kuku – osha, chanja ngozi kidogo ili kuweza kufanya viungo viingie vizuri ndani. Usimtoe ngozi maana itasaidia kumfanya kuku aive vizuri akiwa kwenye moto. Nyunyuzia chumvi, kisha paka kitunguu saumu juu ya kuku vizuri pamoja na kati ya ngozi na nyama. Paka maggi cube kwenye kuku, hakikisha vipande vimewekwa vizuri viungo kisha hifadhi pembeni. Usirundike viungo maana vitazidi na kumfanya mtu ashindwe kula, weka kiasi tu. Hifadhi kuku kwenye jokofu kwa muda wa saa 1 au 2 ili viungo vipate kuingia. Ni vizuri zaidi kama anaweza kukaa kwenye viungo muda mrefu zaidi ili viungo vipate kuingia.
- Washa oven, weka nyuzijoto 200°C (392°F) ili lipate kupata moto vizuri.
- Paka vipande vya kuku mafuta ya kula kwa juu. Mafuta husaidia kuku asiungue na aive vizuri zaidi. Ila hakikisha unatumia mafuta yenye afya - mafuta yanayotokana na mimea na ya samaki.
- Kwenye waya wa oven, panga vipande vya kuku vizuri. Ni muhimu kutumia waya sababu tunataka kuku ajichuje maji yake na aive vizuri hadi ngozi ibaki ikiwa na minofu na laini kwa kuliwa.
Unaweza pia kutumia jiko la mkaa kupika huyu kuku ila usimamizi unatakiwa muda wote ili kuhakikisha moto uko mkali na kuku anaiva pande zote vizuri. Hatua nyingine hazitotofautiana sana.
- Weka wavu wenye vipande vya kuku kwenye oven. Tega muda wa saa 1 ili kuku akauke vizuri.
Kama oven inatoa joto zuri pande zote, kuku ataiva vizuri. Kama joto liko upande mmoja, ni vizuri kugeuza nama ikishaiva vizuri upande mmoja ili ipate kuiva pia upande wa pili.
- Baada ya muda kupita angalia kuku alivyoiva vizuri. Tenga kuku na jirambe.
- Unaweza kula kuku huyu na ugali, wali, ndizi au kama kitafunwa kawaida kama alivyo. Mie nimekula na ndizi mzuzu na viazi vitamu vyenye roast kama vilivyoelezewa hapa.
No comments:
Post a Comment