Thursday, 25 June 2015

JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KUKANDA

Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.
Mahitaji basic:
1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.
Mhitaji extraa:
Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja
1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.
Kwa basic Chapati -Stage 1:
1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)
4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.
Stage 2:
1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)
10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.
Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.
NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.

No comments:

Post a Comment